![]() |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
![]() |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
1. Makubaliano haya wakati wa kukamilika kwa Mradi (ACP) ni maelewano kati ya Wadau wakuu1 kuhusu hali halisi na mapendekezo kutoka Mpango wa Tathmini wa Tanzania (CPE)2. Makubaliano haya yatakuwa msingi wa kuandaa mpango mpya kamambe kwa ajili ya Tanzania (Tanzania Country and Opportunities Paper (COSOP)3 wa IFAD ambao utaelezea mikakati ya muda wa kati (miaka 3 5) pamoja nafasi za uwekezaji nchini Tanzania kutoka mfuko wa IFAD. 2. Makubaliano ya kukamilika kwa Mradi (ACP) yanazingatia mazungumzo na mapendekezo ambayo yametokana na Warsha ya Taifa (CPE National Roundtable Workshop) iliyofanyika Dar es Salaam tarehe 18 19 Novemba 2002, kutumia mambo muhimu yaliyopo katika ripoti ya CPE. Makubaliano ya kukamilika kwa Mradi (ACP) pia yametokana na vipengere mbalimbali vilivyomo katika mada tano ambazo ziliwasilishwa katika Warsha iliyotajwa hapo juu na pia kutokana na matamshi ya Mwenyekiti wa Warsha ya CPE. Makubaliano ya kukamilika kwa Mradi (ACP) yamepangwa kulingana na mada kuu zilizojadiliwa wakati wa Warsha ya CPE. A. Mbinu na Mikakati ya kupunguza Umaskini Vijijini 3. Katika muongo uliopita, IFAD ilitumia mikakati miwili tofauti nchini Tanzania, ambayo inajitokeza katika Ripoti ya Mkakati kwa Tanzania ya mwaka 1993 (CSR) na COSOP ya mwaka 1998. CSR ililenga nchi zilizokuwa maskini kabisa kwa kusaidia miradi ya kilimo ambayo inaboresha uzalishaji na pia inazingatia mahitaji ya watu maskini wa vijijini kwa mfano, kwa kuwapatia maji na huduma za afya. COSOP kwa upande wake huzingatia mikakati iliyo na malengo mapana zaidi ambayo hulenga kuutokomeza umaskini vijijini, mkazo mkubwa ukiwa kwa maskini vijijini ambao wanaweza kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo, wakati wale walio maskini kabisa wakijiondoa kutoka kwenye shughuli za kilimo na kujaribu bahati zao katika sekta nyinginezo au wakitafuta kazi za ajira katika sekta ya kilimo. Kwa kutumia miundombinu ya IFAD ya mwaka 2002 2006 kama msingi, mikakati mbalimbali ya kuutokomeza umaskini pamoja na na malengo ya Taifa ilijadiliwa wakati wa Warsha ya Taifa (CPE) na mapendekezo yafuatayo yalitolewa. |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
4. Suala la 1: Muafaka na Mfumo wa sera za Serikali ya Tanzania Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali ya Tanzania imeandaa mikakati ya maendeleo ya kiuchumi na jamii, ikiwemo Sera ya Taifa ya kuondoa Umaskini (Poverty Reduction Strategy Paper (PRSP), Sera ya Maendeleo Vijijini (the Rural Development Strategy), na Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (the Agricultural Sector Development Programme ASDP. Mikakati hii, pamoja na mambo mengine, inazingatia dira ya Serkali ya Tanzania, miundo mbinu na vipaumbele vya kutokomeza umaskini vijijini na maendeleo ya kilimo vijijini. 5. Mapendekezo: Kuna haja ya Mfuko wa msaada (wa IFAD) kuendeleza muafaka na uendelezaji wa sera kuondoa umaskini vijijini nchini Tanzania. Misaada yote ya IFAD kwa siku za baadaye ni lazima iwe katika misingi ya sera za kutokomeza umaskini vijijini, hususani katika Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP). Njia hii itahakikisha mawasiliano mazuri baina ya miradi mbalimbali ili kuboresha matokeo ya mikakati ya maendeleo na kupunguza gharama za kutoa misaada. 6. Suala la 2: Mbinu za kuutokomeza umaskini vijijini Kulikuwa na muwafaka kwamba jitihada zielekezwe zaidi katika kuwahusisha maskini waliokithiri kama wanufaika wa miradi na programu zinazofadhiliwa na IFAD na kwamba mbinu za kuwapata walengwa hao lazima ziandaliwe. 7. Mapendekezo: Mchango wa IFAD katika kuleta maendeleo lazima uwe na mkakati ulio bayana wa kuwahusisha watu maskini vijijini na kuchambua kwa uwazi na kuandaa mikakati ya kuwafikia watu maskini. Uandaaji wa Miradi na mipango lazima uonyeshe ni mbinu gani zitatumika kuwafikia maskini walengwa na kwamba maskini walengwa kweli ndio waliokusudiwa kunufaika kutokana na miradi na programu inayobuniwa. Hata hivyo ilidhihirika kwamba kuwafikia maskini walengwa ni tatizo zito, na kwa hiyo basi, ni vyema iwapo uandaaji na utekelezaji wa miradi na programu ukazingatia matatizo na matarajio ya mradi/programu. Hii itahitaji maelezo ya kina kuhusu malengo wakati wa hatua mbalimbali za maendeleo ya mradi. Wakati wa utekelezaji, tathmini za mara kwa mara hazina budi kufanyika kuona ni jinsi gani IFAD na wadau wengineo wanawafikia maskini waliokusudiwa. Na mwisho, uchambuzi na tathmini za matokeo ya mbinu za kuutokomeaza umaskini vijijini zilizopendekezwa na COSOP ya mwaka 1988 zitakuwa za manufaa kwa vile zinaweza kutoa mbinu za ziada za kuendeleza mikakati mahsusi na kusaidia kutoa mikakati inayolenga vikundi mbalimbali katika jamii na pia katika sehemu mbalimbali za nchi. 8. Suala la 3: Maana ya Vikundi vya Walengwa Miswada mbalimbali wakati wa kuandaa mradi/programu hutumia maneno maskini na maskini waliokithiri bila kuwatofautisha na jinsi ya kuwafikia. 9. Mapendekezo Tafsiri sahihi ya nani ni maskini na nani ni maskini aliyekithiri lazima zielezwe wakati wa uandaaji wa mradi kwa kuwashirikisha watu maskini vijijini pamoja jamii nzima. Aidha, wakati wa utekelezaji, mbinu za uhakika za kutathmini kuona kwamba vikundi husika vimo kwenye mradi lazima ziandaliwe na kujulikana. Licha ya kutumia mbinu za kuwashirikisha wahusika kwa gharama nafuu, kama vile kupima utajiri wa wahusika, mbinu zinazoweza kutumika ni pamoja na tathmini ya kundi mwanzoni mwa utelekezaji wa mradi, katikati ya utekelezaji wa mradi na mwishoni mwa utekelezaji wa mradi ili kupima ushirikishwaji wa kundi husika na kupima kiwango cha kuuondoa umaskini. 10. Suala la 4: Nyanja/Sekta ndogo na Mkazo Kijiografia Ni wazi kwamba hatua za hivi karibuni za IFAD zenye msisitizo wa nyanja/sekta katika miradi inayofadhiliwa na IFAD (kwa kuacha baadhi ya mipango katika sehemu husika) inaweza ikaboresha mpangilio wa programu na kuimarisha uwezo wa IFAD katika nyanja zilizoteuliwa. Hatua hii pia itaiwezesha IFAD kujihusisha kwa karibu zaidi katika kujadili na kutetea nyanja husika. Pamoja na hayo, kwa kuwa na miradi mingi katika eneo moja lenye maskini wengi zaidi kijiografia kunaweza kukaongezea kwenye wingi wa nyanja mbalimbali na kuwa na matokeo mazuri zaidi ya kuutokomeza umaskini. Aidha,ikumbukwe kuwa na programu nyingi katika eneo moja kijiografia hakuongezi gharama na uendeshaji wake huwa ni nafuu. 11. Mapendekezo: Mwelekeo wa hivi sasa wa kukazania nyanja na sekta ndogondogo hauna budi kuimarishwa katika programu zinazozingatia zaidi hali ya umaskini kama ilivyo katika sera za serikali ya Tanzania. Uwezekano wa kuunganisha nyanja katika eneo moja la kijiografia hauna budi kupewa kipaumbele ili kuhakikisha kwamba misaada ya IFAD haipungui kimaeneo na kinyanja. Mkakati ulio bayana hauna budi kuandaliwa na wadau wote kwa pamoja mwaka moja kabla ya mradi/programu kufikia mwisho ili kuhakikisha kwamba, kifedha na kiuendeshaji, miradi/programu zinakuwa endelevu. 12. Suala la 5: Sera Tanzania ina bahati ya kuwa na mahusiano ya karibu na mashirika mbalimbali yanayotoa misaada. Kuanzia katikati ya miaka ya 1990 mashirika mengi ya kimaendeleo yamewekeza shughuli zao za kiuendeshaji nchini ambapo maamuzi kuhusu matumizi mbalimbali hufanyika. Katika mfumo wa Taifa wa kuutokomeza umaskini (PSRP) serikali na wafadhili wanashirikiana kila mara ili kuchambua mikakati ya nyanja mbalimbali zinazostahili kupewa kipaumbele ili zifadhiliwe. IFAD imekuwa ikizingatia kuzisaidia taasisi tetezi (k.m. mashirika yasiyo ya kiserikali na sekta ya watu binafsi) ambazo hujihusisha zaidi na kuboresha maslahi ya watu maskini, kuwapa uwezo zaidi wa kujiamulia mambo yao na ushiriki mkubwa katika kuandaa sera zao nchini Tanzania. 13. Mapendekezo Wakati tunatambua kuwa mwelekeo wa sera za IFAD kwa ujumla unasisitiza kuwapa uwezo zaidi wawakilishi wa watu maskini, IFAD haina budi kujihusisha vile vile na sera za nchi katika ngazi ya Taifa na vijiji kwa kushauriana na Serikali ya Tanzania pamoja na wadau wengine wa nje katika harakati za kuleta maendeleo. Hatua hii itahitaji kuwa na wawakilishi zaidi wa IFAD katika ngazi ya Taifa na ushiriki kamilifu katika vikundi mbalimbali. Hususani, IFAD haina budi kushiriki na kuchangia katika vikundi mbalimbali vinavyoandaa sera kama vile PRS, UNDAF, FASWOG na ASDP. Pamoja na hayo, ushiriki katika vikundi hivyo kutaiwezesha IFAD kushirikiana na taasisi zingine zinazojihusisha na maendeleo ya kilimo vijijini katika kupanga vipaumbele na uwekezaji wa rasilimali. 14. Suala la 6: Mtazamo mpya wa COSOP nchini Tanzania Siku za nyuma, IFAD ilichukulia COSOP kama waraka wa nchi unaohusika na utekelezaji na undesheshaji. Hata hivyo, COSOP imekuwa chombo muhimu cha IFAD kwa kuwa mshirika wake katika ngazi ya Taifa. 15. Mapendekezo: Uundwaji wa COSOP hauna budi kufanyika kwa ushirikiano baina ya IFAD na Serikali ya Tanzania. Aidha, IFAD pamoja na wadau wengine hawana budi kutumia mtazamo huu mpya wa Tanzania kuhusu COSOP kama kipengere muhimu cha kuendeleza sera za ushiriki zinazojumuisha wadau wote. COSOP haina budi kueleza kinagaubaga mkakati wa IFAD na Serkali ya Tanzania unaolenga kuutokomeza umaskini katika kipindi kifupi na kuona uwezekano wa kuisaidia Tanzania katika malengo na mipango yake ya ya maendeleo kitaifa. Mtazamo mpya wa COSOP nchini Tanzania hauna budi kujadiliwa katika mfumo wa FASWOG na kukamilika ifikapo Juni 2003. B. Ushiriki na Uendelevu 16. Suala la 1: Utaratibu wa Misaada ya Serikali na Kuchangia Gharama Katika mazingira maalum, serikali inaweza kutoa misaada4 kwa viwanda au wazalishaji katika kukabiliana na malengo muhimu ya muda mfupi au mazingira yaliyosababishwa na mazingira maalum. Hata hivyo mara msaada huo unapokoma huwa kuna hatari ya shughuli zilizokuwa zinaendeshwa kusimama vilevile (kwa mfano, pale ambapo wakulima walikuwa wakipewa pembejeo bure kwa ajili ya kuzalisha mbegu kutoka mamlaka inayosimamia mradi, mara baada ya mamlaka hiyo kuacha kutoa msaada basi na shughuli za wakulima kuzalisha mbegu husimama). Vilevile Misaada hiyo ya serikali imekuwa haiwafikii wale walengwa ambao ndio wahitaji zaidi kusaidiwa. Kwa hali hiyo basi, manufaa ya kuchangia gharama yanaonekana wazi zaidi. Kuchangia gharama hupunguza sana hatari ya utegemezi, huongeza uwezekano wa shughuli za mradi kuwa endelevu mara misaada inapokoma na huchangia kuufanya mradi uonekane kuwa ni mali ya walengwa. Hali hii vilevile hupunguza mzigo wa gharama za uendeshaji kutoka serikalini ambayo huwa na bajeti finyu siku zote. 17. Mapendekezo Uchangiaji gharama za uendeshaji uhimizwe kulingana na sera za Serikali (katika sekta za umma na maendeleo ya jamii). Maandalizi na uendeshaji wa uchangiaji gharama lazima yawahusishe walengwa hasa wakati wa kuamua ni kiasi gani walengwa wanapaswa kuchangia na iwapo uchangiaji huo uwe wa kifedha au wa nguvukazi. Mikakati ya uchangiaji gharama lazima wahamasishwe walengwa kwa kiasi kikubwa na mafunzo sahihi yatolewe, ili watu walio maskini vijijini na vikundi vyao watambue nafasi na majukumu yao hasa katika uendeshaji na usimamizi wa shughuli mbalimbali za miradi/programu (O&M). Na mwisho, inapendekezwa kuwa na sera ya aina moja ya uchangiaji gharama itakayotumiwa na IFAD katika miradi inayoifadhili kwa Tanzania nzima na vile vile kuwahimiza wafadhili wengine waifuate sera hiyo. IFAD ina nafasi nzuri ya kutetea sera hiyo ili zitumiwe na wafadhili wengine pamoja na Serkali ya Tanzania katika kuandaa mikakati ya uchangiaji gharama katika harakati za kupambana na umaskini vijijini nchini Tanzania. 18. Suala la 2: Ushirikishwaji Kufikia mwaka 1996, miradi ya IFAD haikuwa imetilia mkazo wa kutosha kwenye ushirikishwaji wa mnufaishwa kwenye ubunifu na utekelezaji mradi. Hakika , taarifa ya COSOP ya mwaka 1998 yasema, kwenye miradi iliyobuniwa awali hoja ya umiliki wa mnufaishwa na haja ya mtizamo shirikishi havikufikiriwa kuwa ni nyenzo kwenye ubunifu, tathimini na utekelezaji wa mradi. Hivi karibuni shughuli zinazofadhiliwa na IFAD zimefanya jitihada za kuwahusisha wanufaishwa, kama vile kwenye upangaji na utumiaji wa zana ya mfumo wa kimantiki (logical framework tool). Hata hivyo mapendekezo kadhaa ya naman na jinsi ya kuzidisha ushirikishwaji yalijadiliwa na kukubaliwa wakati wa warsha ya CPE. 19. Mapendekezo a) Ni muhimu, tangu mwanzo, kukuza uelewa wa pamoja baina ya wadau muhimu
juu ya dhana ya ushirikishwaji, ili kwamba wadau wawe na matarajio yanayooana
na utambuzi wa majukumu yao na wajibu wao makhususi. 20. Suala la 3: Ubunifu wa mradi/programu Miradi na programu zinazofadhiliwa na IFAD zina malengo mapana ya kimaendeleo. Kwa mfano, lengo makhususi la kimaendeleo la mradi hapa Tanzania ni kufufua na kuboresha usalama wa chakula eneo mojawapo ambapo nia yake ni: a) kuboresha uzalishaji chakula ngazi ya familia na kuinua vipato vya
wakulima wadogowadogo; 21. Mapendekezo -Razini malengo ya mradi/programu ili kuhakikisha ukuzaji ufanisi kwenye utoaji na kuwa na matokeo endelevu, wakati huohuo kuhakikisha ushamirishaji wa hali ya juu kwenye miradi na programu zingine husika zinazofadhiliwa na Serikali ya Tanzania (GOT) na wabia wengine katika maendeleo. 22. Suala la 4: Uendeshaji na Utekelezaji wa miradi Serikali ya Tanzania pamoja na wabia wake wakuu wamekuwa wakijitahidi kuongeza uwajibikaji na uwazi kuhusu misaada ya wafadhali wa nje kwa kuzingatia kukubali kwa sera za PRSP na hasa Mkakati wa Taifa kuhusu misaada (Tanzania Assistance Strategy TAS). Lengo ni kuweka misaada ya wafadhili chini ya msimamizi moja kila inapowezekana ili kuwa na muafaka, kupunguza gharama na kuimarisha asasi za taifa. 23. Mapendekezo: IFAD yabidi ijenge na itekeleze kupitia mifumo imara na asasi zilizopo za kitaifa kufuatana na umuhimu wao. Kwenye ngazi ya kieneo, baada ya kukamilika mapitio ya Secretarieti ya eneo, yabidi kuwe na timu ya uwezeshaji ya Tanzania kwenye ofisi ya RAS, na hivyo kuondoa haja ya kuwa na kitengo maalum cha IFAD cha eneo la mradi (PFCUs). Katika ngazi ya wilaya, ni muhimu kuhakikisha ujenzi wa uwezo kwa watumishi wenyeji kushika jukumu la uwezeshaji/uratibu, na pale zilipo, PFCUs, yabidi ziondolewe kabla ya mwisho wa mradi. Kwenye ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya kuna Kitengo cha uwezeshaji chenye jukumu la kuratibu shughuli za mradi katika wilaya ambacho chapaswa kitumike katika kuwezesha shughuli zinazohusiana na IFAD. Chaguo la ushirikiano kiasasi, wabia wanapaswa, kutoishia kwenye mamlaka za Serikali bali hata kuhusisha mashirika ya kijamii na yale ya sekta binafsi, pale ambapo uwezo huo upo na waweza kuchangia ongezeko la thamani. C. Teknolojia ya Kilimo 24. Suala: Miongoni mwa sababu kuu za umaskini na pato duni miongoni mwa watanzaina vijijini ni uzalishaji mdogo katika kilimo utokanao na: pembejeo na desturi duni za uzalishaji mazao ya kilimo na ufugaji; matumizi ya mazao duni ya mifugo; utumiaji mdogo wa teknolojia bora na ya kufaa. Matatizo haya yanachagizwa na miundo dhaifu kiasasi na kiushirika ya ushauri na tafiti za kilimo kwenye ngazi ya kaya na umma, yanayokwamisha ufikiwaji wa malengo yaliyowekwa chini ya Sera ya Taifa ya Kuondoa Umasikini (PRSP) na mpango wa maendeleo wa Sekta ya Kilimo katika kuondoa umasikini vijijini na kuhakikisha usalama wa chakula katika ngazi ya familia. 25. Mapendekezo: a) Utoaji elimu- kuna haja ya kuasasisha tafiti zinazomlenga mteja, ikiwemo
kuchukua takwimu za teknolojia sanifu na bora na kuwahusisha wakulima
maskini kabisa kwenye kutathmini teknolojia zilizopo na mpya. Wakulima,
mashirika ya jamii ya kiraia na sekta binafsi zapaswa kujihusisha katika
kuendeleza tekinolojia mpya. D. Usimamiaji na Tathimini 26. Suala: Miradi na programu zote zinazofadhiliwa na IFAD nchini Tanzania imejumuisha mfumo wa usimamiaji na tathmini (M&E). Hata hivyo, kama inavyoonyesha kwenye nyaraka za mwaka 1998 za fursa na mikakati ya Tanzania, utekelezaji wa mifumo ya usimamiaji na tathmini (M&Es) umekuwa hautoshelezi kwa sababu nyingi ambazo zinafahamika wazi. Katika miaka ya hivi karibuni, juhudi za makusudi zimefanywa kuboresha utendaji wa mifumo ya usimamizi na tathimini (M&E) kwa kuwashirikisha wanufaika. Washiriki wa warsha ya taifa ya CPE wameafiki umuhimu wa usimamizi na tathmini kama nyenzo ya utawala, na wameafikiana juu ya mapendekezo yafuatayo. 27. Mapendekezo a) kutoka kwenye msukumo wa ugavi (supply-driven) kwenda kwenye mvuto
wa uhitaji (demand-led) juhudi za makusudi zapaswa ziwe kwenye kufunza
jamii kuhusishwa kwenye shughuli za usimamizi na tathmini (M&E) na
kuwafanya wamiliki wa njia za usmimizi na tathimini (M&E). E. Masuala ya Kijinsia 28. Suala: Dhana na umuhimu wa kuwahusisha maskini kwenye kitovu cha hatua za maendeleo, sio kama washiriki tu bali kama wabia makini, vipo kwenye msingi wa mitazamo na fikra za mradi uliopo na mpya wa IFAD. Suala hili pia linagusa masuala mbalimbali yahusuyo jinsia kwa ujumla, hususan juu ya haja ya kutafuta njia na namna ya kukuza uhusishwaji wa kimafanikio wa wanawake kwa ujumla na hasa familia zinazoendeswa na wanawake kwenye hatua za kimaendeleo. 29. Mapendekezo a) Uchanganuzi wa jinsia wapashwa ujumuishwe kwenye ubunifu programu
na shughuli za usimamizi na tathmini(M&E). Endnotes 1. Wadau wakuu ni pamoja na Serikali ya Tanzania, (ikiwakilishwa na Wizara ya Kilimo na Chakula, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha, Wizara ya Maji na Maendeleo ya Mifugo na Ofisi ya Makamu wa Rais), Mamlaka za Mikoa na Wilaya, (Dodoma, Kagera, Mara, Mbeya) Miradi inayofadhiliwa na IFAD (AMSDP, KAEMP, MARA-FIP, PIDP, na WSHPMA) , Taasisi Shiriki UNOPS, mashirika yasiyo ya Kiserikali ikiwemo Pride, na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na miradi ya maendeleo zikiwemo FAO, UNDP, WFP, na Benki ya Dunia, Mfuko wa Kibeljiji inayoshughulikia Uhai, pamoja na IFAD (ikiwakilishwa na Kitengo cha Nchini za Mashariki na Kusini mwa Afrika pamoja na Ofisi ya Tathmini) 2. Ulioshughulikiwa na ofisi ya IFAD ya Tathmini katika mwaka wa 2001/2002. 3. Maandalizi ya COSOP ni jukumu la Kitengo cha IFAD kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika. 4. Malipo yanayofanywa na serikali
kwa wazalishaji au wasambazaji kiwandani ili kuzuia kudidimia kwa kiwanda
(k.m. kutokana na uzalishaji usioleta faida) Todaro katika
Economic Development. Misaada inaweza kusababisha uzalishaji mkubwa
au matumizi yasiyo ya faida ya pembejeo na kwa kawaida mashirika makubwa
na yenye kujiendesha kifaida huziba pengo katika viwanda vinavyojiendesha
kwa hasara. Misaada hii ya serikali inaweza kuwa mzigo mkubwa kwa walipa
kodi. Bawn na Tolbert katika Investing in Development.
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
| Back | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||